Jeremiah 22:10-12

10 aUsimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;
badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu
yule aliyepelekwa uhamishoni,
kwa sababu kamwe hatairudia
wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.
11 bKwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu
Shalumu ndiye pia anaitwa Yehoahazi.
mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena.
12 dAtafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.”

Copyright information for SwhNEN